Thursday, November 30, 2017
Saturday, November 25, 2017
Thursday, November 16, 2017
Wednesday, November 15, 2017
Monday, November 13, 2017
Saturday, July 29, 2017
JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI
1.
Sulphonic(LABSA)
2.
Slec
3.
Pafyumu (lemon)
4.
Rangi (kijani/ nyekundu/ blue)
5.
Chumvi nzuri ya
mawe.
6.
Glycerin
7.
Soda ash light.
8.
Formalin na alka.
9.
Maji yaliyokuwa
safi .
10.
Chombo zaidi ya
lita 25.
JINSI YA KUTENGENEZA
1. Chukua sulphonic
1 lita moja weka katika chombo chako cha
kutengenezea(lita 25) .
2. Kisha chukua slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka sulphonic kisha changanya kwa pamoja.
3. Chukua soda
ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine pembeni , kisha
chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako chenye mchanganyiko wa sulphonic
na sles
weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10 kuwa makini kwasababu utavimba sana.
4. Kisha weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi
kutokana na rangi unayoitaka lakini
angalia isizidi sana koroga tena vizuri.
5. Kisha chukua glycerin
vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo
chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana .
6. Kisha weka 25ml
yani kwa kiasi unachotaka pafyumu
(lemon) , hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri.
7. Koroga chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu kama vijiko 6 ya chai
kisha mimina katika mchanganyiko wako na malizia kiasi cha maji mpaka kufikia
lita 25 ambazo ni wastani kabisa.
NB , Chumvi
ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwahiyo kuwa makini sana.
8. Kisha weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuweka
formalin
kisha koroga tena vizuri. (alka na formalin sio lazima sana hata kama
hautavitumia sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).
ANGALIZO
1.
Mchanganyiko
wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa makini.
2.
Kuna baadhi ya
malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga kama MASKI NA GLOVES.
Tembelea www.gawazabrain.blogspot.com NA gawazaTV - youtube kwa mafunzo kwa vitendo. 0684-863138.
kwa matatizo tuwasiliane usisite kwa hili wakati wowote hata kama ni usiku
Sunday, July 16, 2017
Friday, June 30, 2017
HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA
1. TUMIA UJUZI ULIO NAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?
Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe
2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?
Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening.
3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo
4. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE.
Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa.
Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia
5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kadhalika.
6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustarehe.
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?
7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.
8. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara.
9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi.
10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza
11. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara
12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika
13. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
- Maonyesho ya biashara
- Magazeti,
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
- Kwa marafiki.
14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako
15.
MWISHO USIENDELEE KUSUBIRI ANZA SASA BIASHARA YAKO