1.
Sulphonic(LABSA)
2.
Slec
3.
Pafyumu (lemon)
4.
Rangi (kijani/ nyekundu/ blue)
5.
Chumvi nzuri ya
mawe.
6.
Glycerin
7.
Soda ash light.
8.
Formalin na alka.
9.
Maji yaliyokuwa
safi .
10.
Chombo zaidi ya
lita 25.
JINSI YA KUTENGENEZA
1. Chukua sulphonic
1 lita moja weka katika chombo chako cha
kutengenezea(lita 25) .
2. Kisha chukua slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka sulphonic kisha changanya kwa pamoja.
3. Chukua soda
ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine pembeni , kisha
chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako chenye mchanganyiko wa sulphonic
na sles
weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10 kuwa makini kwasababu utavimba sana.
4. Kisha weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi
kutokana na rangi unayoitaka lakini
angalia isizidi sana koroga tena vizuri.
5. Kisha chukua glycerin
vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo
chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana .
6. Kisha weka 25ml
yani kwa kiasi unachotaka pafyumu
(lemon) , hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri.
7. Koroga chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu kama vijiko 6 ya chai
kisha mimina katika mchanganyiko wako na malizia kiasi cha maji mpaka kufikia
lita 25 ambazo ni wastani kabisa.
NB , Chumvi
ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwahiyo kuwa makini sana.
8. Kisha weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuweka
formalin
kisha koroga tena vizuri. (alka na formalin sio lazima sana hata kama
hautavitumia sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).
ANGALIZO
1.
Mchanganyiko
wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa makini.
2.
Kuna baadhi ya
malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga kama MASKI NA GLOVES.
Tembelea www.gawazabrain.blogspot.com NA gawazaTV - youtube kwa mafunzo kwa vitendo. 0684-863138.
kwa matatizo tuwasiliane usisite kwa hili wakati wowote hata kama ni usiku
iko pw mkuu thnx
ReplyDeleteNaomba kujua Lita moja kwa wastani inauzwa being gani
ReplyDelete1000
Deletenimeipenda sana hii. asante sana kwa somo zuri
ReplyDeleteVery interesting ,but put it in english
ReplyDeleteImekaa poa sana,wapi yanapatikana hayo material
ReplyDeleteKama upo dar k/koo utapata
DeleteSlec unaweka kiasi gani mbona hujaonesha
ReplyDeleteNimevutiwa na somo hilo.
ReplyDeleteJe hizi malighafi zinapatikana wapi?
ReplyDeleteNaitaji kujifunza nitakupataje
ReplyDeleteAisee,vijiko 6 vya chumvi nimefanya but nimeingia hasara,coz imebaki kuwa maji kabisa ,naibadilishaje ili iwe nzito???
ReplyDeleteIkitokea ivo tena iache kwa siku kadhaa itabadilika na kua nzito
DeleteOngeza slice kufanya kuwa nzito
DeleteKwa Lita 20 chumvi ni 500g yaani kile ki packet kimoja cha chumvi kinachouzwa 500
DeleteSafi sana
ReplyDeletesafi sana. kuzaliwa maskini si tatizi, kufa maskini ndiomtatizo. sasa ni watu kuamka na kuukataa umaskini.
ReplyDeletenimeipenda sana hiyo
ReplyDeleteKwa Lita 40 je inakuwaje vipimo vyake na VP kwa chumvi ya unga
ReplyDeleteSomo zuri sana
ReplyDeleteNaomba nitumie bro kwenye email yang
ReplyDeleteNitumie bro kwenye email yang
ReplyDeleteKwa hapo nliv soma naona kam umetengeneza lita 20 na sio lita 25 na vpimo umesem ni lita 25 sas meshindwa kuelewa hapo
ReplyDeleteEnter your comment...JAMANI HAYO MATERIALS YA KUTENGENEZA YANAPATIKANA WAPI?
ReplyDeletejammani material yanapatikana kwenye maduka gani
ReplyDeleteInategemea na mkoa, ukiyahitaji sana naomba nitafute kwa namba 0788077444 hata mikoani tunatuma
DeleteMaterial bei gani
DeleteKweli mzee lakini waweza kutumia kiingereza kwa yale majina ya chemicals maana kiswahili kilinipita Left side mzee
ReplyDeleteElimu nzuri ya ujasiriamali,mda mwngne tunahitaj kujitoa kwa faida yetu lakn pia na kwa jamii kiujumla.
ReplyDeleteUtengenezaji wa Sabuni ya maji na shampoo ya nywele ni sawa?
ReplyDeleteNataka kutengeneza shampoo ya nywele?
Good lesson
ReplyDeleteVery interesting
ReplyDeleteMaterial s hayo yanapatikani kwenye maduka gani nipo makambako njombe please naomba msaada nimelipenda someone lako
ReplyDeleteMoshi kilimanjaro,material tunapata wapi
ReplyDeleteIngekuwa vizuri tungejua mahitaji yanapatikana wapi aidha maduka ya kawaida au supermarket ingekuwa fresh Zaid
ReplyDeleteSomo nzuri mno
ReplyDeleteKipi kinafanya rangi ichuje (isionekane) baada ya mda flani
ReplyDeletehiyo formalin na alika inafanyanga kazi gani , hata isikue na umhimu, mimi nafunga plodder machine kwa Bar soap, na pia natumia mixer to saponify, je inaweza kukuwa rahisi kuitumia formula yako.
ReplyDeletenaomba kujua kama umetengeneza sabuni na haija zito ila inatoa povu vzuri kabisa nawezaje kuifanya iwenzito ili nisile hasara??
ReplyDelete