1.
Sulphonic(LABSA)
2.
Slec
3.
Pafyumu (lemon)
4.
Rangi (kijani/ nyekundu/ blue)
5.
Chumvi nzuri ya
mawe.
6.
Glycerin
7.
Soda ash light.
8.
Formalin na alka.
9.
Maji yaliyokuwa
safi .
10.
Chombo zaidi ya
lita 25.
JINSI YA KUTENGENEZA
1. Chukua sulphonic
1 lita moja weka katika chombo chako cha
kutengenezea(lita 25) .
2. Kisha chukua slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka sulphonic kisha changanya kwa pamoja.
3. Chukua soda
ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine pembeni , kisha
chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako chenye mchanganyiko wa sulphonic
na sles
weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10 kuwa makini kwasababu utavimba sana.
4. Kisha weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi
kutokana na rangi unayoitaka lakini
angalia isizidi sana koroga tena vizuri.
5. Kisha chukua glycerin
vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo
chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana .
6. Kisha weka 25ml
yani kwa kiasi unachotaka pafyumu
(lemon) , hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri.
7. Koroga chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu kama vijiko 6 ya chai
kisha mimina katika mchanganyiko wako na malizia kiasi cha maji mpaka kufikia
lita 25 ambazo ni wastani kabisa.
NB , Chumvi
ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwahiyo kuwa makini sana.
8. Kisha weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuweka
formalin
kisha koroga tena vizuri. (alka na formalin sio lazima sana hata kama
hautavitumia sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).
ANGALIZO
1.
Mchanganyiko
wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa makini.
2.
Kuna baadhi ya
malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga kama MASKI NA GLOVES.
Tembelea www.gawazabrain.blogspot.com NA gawazaTV - youtube kwa mafunzo kwa vitendo. 0684-863138.
kwa matatizo tuwasiliane usisite kwa hili wakati wowote hata kama ni usiku