JINA LA MWANDISHI : Mohammed
A. Gawaza
MAWASILIANO :
0684-863138 / 0718- 567689 /
0743 - 214416
Youtube :
Gawaza Online TV ( G.O.T )
JINA LA KITABU : MJASIRIAMALI MBUNIFU
JINA LA MAKALA : UTENGENEZAJI WA SABUNI MBALIMBALI
SABUNI
{ SOAP }
Maana
ya sabuni
Nibidhaa ambayo hutumika kwa
matumizi mengi sana katika jamii zetu husika, Ni bidhaa chache sana zilizo
muhimu na hutumiwa sana kwa matumizi kama sabuni .
Na
hii imethibitishwa katika kila hatua yako ya maisha lazima utumie sabuni ,
utotoni ulitumia sabuni na mpaka sasa.
Tangu
ilipotengenezwa kwa mara ya kwanza imeachwa kuwa ni bidhaa muhimu inayotumiwa
kila siku.
Mwana kemia mmoj aliwahi kusema
katika karne ya 19 kwamba “ Utajiri na ustaarabu wa taifa huamuliwa na kiasi
cha sabuni kinachotumniwa”
MATUMIZI
MBALIMBALI YA SABUNI
Matumizi makuu ni kuondoa Uchafu wa aina
yeyote , matumizi ni kama ifuatavyo;
§
Kufulia
§
Kuoshea
vyombo
§
Kusafishia
vitu mbalimbali mf. sinki
§
Kuogea
§
Kunawia
mikono N.K
0 comments:
Post a Comment