Home »
» JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA / DETERGENT SOAP
JINA LA MWANDISHI : Mohammed
A. GawazaMAWASILIANO :
0684-863138 / 0718- 567689 /
0743 - 214416 Email :mgawaza12@gmail.com Youtube :
Gawaza Online TV ( G.O.T ) Blog : www.gawazabrain.blogspot.comJINA LA KITABU : MJASIRIAMALI MBUNIFUJINA LA MAKALA : UTENGENEZAJI WA SABUNI YA UNGA
(DETERGENT SOAP)
SABUNI
YA UNGA / DETERGENT SOAP Ni sabuni
ambayo inapendwa na hutumika zaidi majumbani katika matumizi ya kawaida. MALIGHAFI
ZA SABUNI YA UNGA ( DETERGENT SOAP)
Hizi malighafi ni kama mwongozo wa kutengeneza sabuni kiasi (kilo 4,8
n.k) ndogo lakini unaweza ukazidisha kupitia hivi na kupata sabuni nyingi
zaidi,§ Sulphonic acid – Hutumika
kuzalisha bidhaa nyingi za viwandani mf; dye. Sabuni n.k
§ Sodium Sulphate–Hufanya
kazi kama chumvi katika kuzalisha sabuni.
§ Optical brighter
- Hufanya sabuni iwe ina ng’aa.
§ Nasa -
§ Soda ash
– Ni kibebeo cha sabuni ili ikamilike mfano unga , majivu.
§ Perfume - Hufanya sabuni kuwa na harufu nzuri.
§ Rangi
– Kwa ajili ya kubadilisha rangi mfano kijani, blue, n.k
§ Hydrogen peroxide - Hii
hufanya sabuni kuwa mara mbili ya uliyotengeneza mfano kilo 5 kuwa 10.
§
Sodium
metasilicate – Hii hutumika katika kukausha maji
katika sabuni na ikitumiwa huwa sabuni
haianikwi.
§
VIFAA VITUMIKAVYO § Beseni/sufuria
kubwa safi
§ Mwiko
mrefu
§ Gloves
§ Ndoo
safi
§ Maski
§ Kipimio
JINSI
YA KUTENGENEZA ( 5 kg) 1) Tafuta
beseni kubwa na safi kisha chukua Sulphonic acid ( Lita moja 1) na mimina
katika beseni lako.
2) Chukua Sodium sulphate (3kg) kisha mimina katika beseni lako ambalo
lina sulphonic acid.( koroga dakika 5) 3) Mimina
BRIGHTER vijiko 6 katika mchanganyiko wako.
4) Mimina
NASA vijiko 16 changanya kwa pamoja kwa dakika Zaidi ya 5
( koroga dakika 5)5) Mimina
SODA ASH LIGHT kg5 katika mchanganyiko
wako kisha changanya kwa dakika Zaidi ya 5.(
koroga dakika 5) 6) Kisha
chukua pafyumu yako kiasi kidogo yenye harufu nzuri na mimina katika
mchanganyiko wako na changanya kwa dakika 5-6( koroga dakika 5) 7) Maji
kidogo 500ml na mimina katika mchanganyiko wako wa sabuni ya unga .
8) Hapo
utaona kama unga uliomwagiwa maji , kisha utaanika sabuni yako kwa muda wa
masaa 4-5 katika kivuli.
9) Na
mwisho kabisa unatakiwa kuweka deteregent booster ( Hydrogen peroxide) kwa
ajili ya kuongeza wingi wa sauna yako.
NB: Tahadhari ukianika juani baada
ya kutengenezwa sabuni yako itayeyuka na
kama hutaki kuanika kivulini basi itatakiwa utie SODIAM METASILICATE hii
hufanya kazi ya kukausha maji.
Safi sana kwa somo zuri ulilo litoa sehemu hii, piah nina shida nawewe GAWAZABRAIN 0621146815 namba yangu
ReplyDelete