Friday, July 20, 2018

MALIGHAFI ZA SABUNI YA MICHE / MATERIALS by MOHAMMED GAWAZA


MALIGHAFI ZA SABUNI YA MICHE / MATERIALS



     Hizi malighafi ni kama mwongozo sabuni ndogo lakini unaweza ukazidisha kupitia hivi na kupata sabuni nyingi zaidi,
§  Caustic Soda   (450g )
§  Slec/ unga low  ( nusu kilo )
§  Pafyumu(Rose, lemon, kasablanka n.k )vijiko kadhaa
§  Sodium silicate
§  Maji safi chupa 4 za soda
§  Mafuta(mawese, mise, nazi, ubuyu)- (lita moja) na  Mashudu kiasi
VIFAA VITUMIKAVYO
§  Beseni/sufuria kubwa safi / Ndoo safi
§  Mwiko mrefu
§  Gloves
§  Mask
§  Kipimio 
§  Soap moulder

JINSI YA KUTENGENEZA

1)    Andaa beseni safi kisha mimina maji chupa 4 za soda.
2)    Weka Caustic soda 450g koroga mpaka ziyeyuke (Hii ipo katika hali ya chengachenga,ukiweka  maji yatakuwa yamoto hivyoutakoroga ili maji yapoe)
3)    Weka mafuta yako lita moja 1  na mashudu kisha koroga kwa dakika kadhaa.
4)    Weka sodium silicate kisha koroga tena kwadakika kadhaa mpaka upate uzito unaotaka
5)    Na mwisho utaweka sles/ unga low nusu katika mchanganyiko wako kisha koroga tena vizuri mpaka upate mchanganyiko mzuri zaidi na
6)    Kisha utaweka pafyumu yako vijiko 4-5 kutokana na harufu unayoitaka .
7)    Hapo utakuwa tayari umeshamaliza kutengeneza , kisha weka katika chombo(soap moulder)hapo utasubiri siku moja au 2 sabuni yako itagande naitakuwa tayari kwa matumizi.

0 comments:

Post a Comment